Jinsi Ya Kumuapproach Mwanamke Katika Gari La Abiria
Hello reader wa IBRAH LIVE! Somo la leo ukimaliza kulisoma nataka ukajaribu angalau mara moja. Najua kuna baadhi ya watu ambao washawahi hujaribu na kufaulu (kawaida unafaulu asilimia 100 kila wakati), so somo lenyewe ni kuapproach mwanamke katika gari la usafiri la abiria.
Ok, hebu tuanze hivi, ni mara ngapi ushawahi kuingia katika basi ukakutana na mwanamke mrembo ukamtamani? Ama ni mara ngapi ukiwa ndani ya gari ushawahi kumwona mwanamke mrembo ameingia na kukaa mbele yako? Ni mara nyingi. Mambo kama haya hutokezea kila siku. Mwanzo kila siku unapoabiri basi huwa unakutana na wanawake tofauti tofauti na warembo. Na je, unajua mbinu ya kuwaaproach uanze mazungumzo? Somo letu litafafanua kwa upana.
Wanawake wakiwa ndani ya magari ya usafiri huwa rahisi kuwaaproach tofauti na sehemu nyingine unazozijua. Hii ni kwa sababu ya mambo haya:
1. Kinga zake ameziweka chini. Katika gari za usafiri mwanamke huwa hayuko katika hali ya kutangamana, so hatakuwa na mawazo katika akili yake kama vile anavyokuwa katika kilabu. Mfano hafikirii mbinu za kukabiliana na wanaume wanaoudhi ama kuwa na wasiwasi wa kwanini hakuna mtu mpaka sahizi amemuaproach. Nguvu zake zote katika gari la usafiri huwa zimetulia ukilinganisha na wakati ameenda kula bata na marafiki zake usiku. Katika hali hii huwa ni rahisi kumuaproach na anaweza kuungana na wewe kirahisi bila matatizo.
2. Gemu huwa ya juu. Katika magari ya usafiri wanawake ni wengi mno. Kila siku ukisafiri utakutana na wanawake tofauti. Wale ambao utakutana nao leo, si wale ambao utakutana nao kesho. Hii inamaanisha kuwa kadri utakapokuwa ukisafiri ndipo utakapokuwa na nafasi nzuri ya kuchagua mwanamke unayetaka wewe.
3. Una mstari ambao unafanya kazi kila wakati. Kuanza mazungumzo na mwanamke ni rahisi katika magari ya usafiri. Sentensi kama, "Unasafiri ukielekea wapi?" Tayari inaweza kuamsha mazungumzo yasiyokuwa na mwisho.
Ok. Hapo juu tumeonyesha sababu muhimu ambazo zinafanya kuapproach mwanamke katika gari la usafiri kuwa rahisi kuliko zote.
Kuna aina tatu za kumtambua mwanamke abiria. Nazo ni kama zifuatazo:
Hali #1 Mumesimama nje ya gari la usafiri unangojea kuingia ndani ukamwona mwanamke unayempenda. Katika hali hii mara nyingi hutokea katika basi. Abiria wote wako nje wanangojea kuabiri basi, halafu ghafla ukakutana na mwanamke unayevutiwa. Hatua ya kufanya hapa ni rahisi. Unachotakiwa kuanza ni kwenda hadi pale alipo, simama karibu yake halafu umwambie, "Waah, leo abiria ni wengi/wachache. Hivi unaelekea wapi?" Hapa atakujibu bila wasiwasi wowote sababu kinga zake zote ameziweka chini (sababu tumeeleza hapo juu).
Akikujibu usimalizie hapo, mwambie pia wewe unaelekea wapi. Katika mazungumzo yenu hakikisha unaongea mada ambazo zinazungumzia usafiri, usiingize siasa wala michezo. Halafu kuaproach hivi lazima uwe mtu asiyemwoga. Kama unatatizika na uoga wa kutojiamini ingia hapa. [Soma: Jinsi ya kuondoa uoga wa kuaproach mwanamke]
Sasa mazungumzo yenu hayaishi hapo nje, lazima uingie ndani ya gari. Sasa hapa kuna changamoto kidogo. Kama unaingia ndani ya gari ambalo kiti unajichagulia mwenyewe utakuwa umefaulu kumnasa. Kama tayari mumepewa tiketi ambayo kila mtu ameandikiwa kiti chake itakuwa vigumu kuendelea na appraoch kwa huyu mwanamke kama kiti chako ni nambari 12 na yeye ni 35.
Post a Comment